Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

ZOEZI LA UHAKIKI NA UHUISHAJI WA VYETI VYA USAJILI WA TAASISI ZOTE ZA DINI

  TANGAZO

Ofisi ya Msajili wa Jumuiya, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, itaendesha Zoezi la Uhakiki na Uhuishaji wa Vyeti vya Usajili wa Taasisi zote za Dini zilizosajiliwa katika  Wizara hii.

Zoezi kwa taasisi zilizoko Dar es Salaam, Pwani na Morogoro  limeanza  Novemba 21,  hadi  Desemba 3, 2022 katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Dar es Salaam kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni.

Viongozi wa taasisi za kidini wafike na

·         Cheti cha Usajili na Nakala ya Cheti hicho,

·         Katiba na Kanuni zinazotumika 

·         Taarifa za Mapato na Matumizi na Utendaji za Miaka mitano   

·         Uthibitisho wa Malipo ya Ada kwa miaka mitano, na

·          Ada ya cheti kipya shilingi 100,000/=.

Taasisi za Kidini zitakazoshindwa kushiriki zitahesabika hazipo hai hivyo kujiondoa  zenyewe kwenye Kazindata ya Jumuiya zilizosajiliwa.

Huduma za Ulipaji wa Ada zitatolewa, Kanda itakayofuata ni Kaskazini na ratiba ya Kanda nyingine itatangazwa baadae.

Kwa ufafanuzi piga namba  0734712744, 0734712745 au barua pepe rs@moha.go.tz.

Imetolewa na:

MSAJILI WA JUMUIYA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI