generica viagra

News

HOTUBA YA MGENI RASMI, WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MHE. MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU, MB. WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO WA MWAKA WA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA MAGEREZA BWALO KUU LA MAAFISA MAGEREZA - UKONGA, D’SALAAM, TAREHE 17 MACHI, 2017

Friday, March 17, 2017

HOTUBA YA MGENI RASMI, WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI
MHE. MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU, MB. WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO WA MWAKA WA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI
LA MAGEREZA BWALO KUU LA MAAFISA MAGEREZA - UKONGA, D’SALAAM, TAREHE 17 MACHI, 2017
 

 • Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma A. Malewa,
 • Kamishna wa Fedha na Utawala,
 • Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Magereza,
 • Wakuu wa Magereza wa Mikoa Tanzania Bara,
 • Wakuu wa Vyuo vya Magereza,
 • Mkuu wa Kikosi Maalum,
 •  Mkuu wa Bwawani Sekondari,
 • Viongozi mbalimbali mliopo,
 • Wageni Waalikwa,
 • Waandishi wa Habari,
 • Mabibi na Mabwana.

 
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufika siku hii ya leo tukiwa na afya njema. Nashukuru pia kwa kupata fursa ya kuwa Mgeni Rasmi katika hafla hii ya ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara.
 
Ndugu Kamishna Jenerali,
Kwa kuwa huu ni mkutano wangu wa kwanza wa aina hii kwa uongozi mpya wa Jeshi, nitumie fursa...

AWAMU YA KWANZA YA WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAHAMIA DODOMA MAKAO MAKUU YA NCHI TAREHE 27 FEBRUARI, 2017

Wednesday, March 1, 2017

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
 
TAARIFA KWA UMMA
AWAMU YA KWANZA YA WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAHAMIA DODOMA MAKAO MAKUU YA NCHI TAREHE 27 FEBRUARI, 2017
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inapenda kuwafahamisha Umma kuwa, Awamu ya Kwanza ya Watumishi wa Wizara wamehamia Makao Makuu ya Nchi, Dodoma tarehe 27 Februari 2017.
Awamu ya kwanza inajumuisha Watendaji Wakuu wa Wizara akiwemo Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Naibu Waziri, Katibu Mkuu pamoja na Naibu Katibu Mkuu.
Wamo pia baadhi ya Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na wasaidizi wao.
 Aidha, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pia inawajulisha kuwa kwa sasa Ofisi zetu zitakuwa katika majengo ya Asha Rose Migiro Foundation katika Chuo Kikuu cha Dodoma na Anuani mpya itakayotumiwa mkoani Dodoma ni:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
S.L.P 2916,
DODOMA
Simu: +255 262323189/262320186
             Barua pepe:ps@moha.go.tz
          Website: www.moha.go.tz
 
Imetolewa na:
Christina R. Mwangosi
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
28/2/2017

MSAMAHA WA RAIS KWA WAFUNGWA KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA, TAREHE 9 DESEMBA, 2016

Friday, January 6, 2017

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
 
MSAMAHA WA RAIS KWA WAFUNGWA KATIKA
KUADHIMISHA MIAKA 55 YA UHURU WA
TANZANIA BARA, TAREHE 9 DESEMBA, 2016
 
Katika kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba, 2016 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa wafuatao:-
 

 1. Wafungwa wote wamepunguziwa moja ya sita (1/6) ya vifungo vyao zaidi ya punguzo la kawaida linalotolewa chini ya kifungu 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara ya 2 (i-xx).

 

 1. Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama UKIMWI, KIFUA KIKUU (TB) na SARATANI (CANCER) ambao wako kwenye “terminal stage”. Wafungwa ambao wamethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

 

 1. Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi ambao umri huo umethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

 

 1. Wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya.

 

...

Hotuba ya Mgeni Rasmi

Friday, February 19, 2016

HOTUBA YA MGENI RASMI, WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MHE. CHARLES M. KITWANGA, MB AKIFUNGUA KIKAO CHA KAZI CHA  MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI UKUMBI WA JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVENTION CENTRE, DAR ES SALAAM  TAREHE 18 – 19 FEBRUARI 2016

 • Inspekta Jenerali wa Polisi, Ndugu Ernest Jumbe MANGU,
 • Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdurahman KANIKI,
 • Makamishna wa Polisi,
 • Naibu Makamishna wa Polisi,
 • Wajumbe wa Mkutano,
 • Waandishi wa Habari,
 • Wageni waalikwa,
 • Mabibi na Mabwana.

 
Habari za asubuhi!
Heri ya Mwaka Mpya!
Napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana hapa leo hii. Pili, natumia nafasi hii kumshukuru Inspekta Jenerali wa Polisi ndugu Ernest Mangu kwa kunipa heshima hii ya kuwa Mgeni Rasmi katika Kikao hiki muhimu. Kupitia hafla hii ninapata fursa ya kuzungumza na na viongozi wote waandamizi wa Jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi ambao ni wasimamizi wakuu wa kazi za Polisi. Ninawapongeza sana kwa utaratibu huu mliojiwekea...

Meja Jenerali Rwegasira ataka Polisi wenye tabia ya kuwabambikizia kesi wananchi wachukulie hatua kali

Wednesday, January 27, 2016

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amewataka viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi nchini kuhakikisha wanawachukulia hatua kali askari polisi wenye tabia ya kuwabambikizia kesi wananchi.
Meja Jenerali Rwegasira alisema Jeshi hilo lina sifa nzuri nje ya nchi pamoja na hapa nchini lakini kuna baadhi ya askari wasiowaadilifu wanawaonea wananchi mitaani wasiokuwa na hatia kwa kuwabambikizia kesi ambapo wanalitia doa jeshi hilo.
“Jeshi letu lina sifa nzuri, niliwahi kwenda nchini Kenya nikaambiwa Jeshi la Polisi Tanzania lina maadili kwani hata likimkamata mhalifu linafuata sheria na utaratibu na sio kutumia nguvu kubwa kama yalivyo majeshi mengine,” alisema Rwegazira.
Rwegasira aliongeza kuwa, amefurahishwa sana na utendaji kazi wa jeshi hilo na kutaka kuongeza umakini zaidi ili kuliletea sifa zaidi jsehi hilo na yeye yupo karibu nao katika kuliendeleza jeshi hilo ili liweze kufanya kazi kwa weledi.
Alisema kuwa ni askari wachache mno wenye tabia hiyo ya kuwabambikizia kesi wananchi na kutofuata sheria za jeshi, hivyo kazi ya kupambana na askari hao inawezekana endapo viongozi wa jeshi wakiamua kulifanyia kazi.
“Utendaji kazi wenu ni mzuri, nawapongeza sana hasa mlivyosimamia uchaguzi mkuu vizuri kwani wananchi wengi walikuwa na wasiwasi kuhusu usalama wao katika kipindi cha uchaguzi, lakini mlisimama imara kuhakikisha uchaguzi unamalizika salama,” alisema Rwegasira.
Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa...

Pages

Subscribe to
Back to Top