generica viagra

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari Kuhusu Ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni Aliyoifanya Katika Ofisi Kuu Ya Uhamiaji Zanzibar Tarehe 11 Januari, 2016

Friday, January 15, 2016

 
Naibu waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amewataka Maafisa Uhamiaji kufuata sheria wakati wa kutekeleza zoezi la kuwabaini raia wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi hapa nchini kinyume cha sheria na kulitekeleza zoezi hilo kwa uadilifu na weledi.
Mheshimiwa Masauni aliyasema hayo wakati akizungumza na Viongozi na Maafisa Uhamiaji katika Ofisi kuu ya Uhamijai Zanzibar iliyopo eneo la Kilimani alipofanya ziara kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Ofisi hiyo.
Amesema kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Uhamiaji itaimarisha zoezi la kuwabaini raia wa kigeni wanaoishi na kufanyakazi nchini bila vibali halali na kuwa itawachukulia hatua za kisheria wote watakaokamatwa ikiwa ni pamoja na kuwarejesha kwao.
Hata hivyo alisema wageni wenye vibali halali vya kuishi na kufanya kazi hawatabughudhiwa kwa vyovyote vile na kuwa Afisa atakayekiuka maagizo haya atachukuliwa hatua za kinidhamu.
“Tanzania kama zilivyo nchi nyingine duniani  tunapenda wageni, tunajua kwamba watalii  na wawekezaji  wanatoa mchango mkubwa katika kuinua uchumi wa taifa letu, hivyo hatuwezi kuwafukuza ama kuwanyanyasa kama wako nchini kihalali” alisema Bw. Masauni.
 Aidha amewataka maafisa wa Uhamijia kutotumia zoezi hilo kwa manufaa yao na kuwa yeyote atakae bainika kutumia zoezi hilo kinyume na agizo la serikali atashughulikiwa.
Amesema kuwa sheria zilizopo nchini ni kwa ajili ya manufaa ya watu wote  hivyo ni lazima kila mtu aziheshimu na kuwa Serikali haina lengo la kutumia sheria hizo kukandamiza wageni.
Pamoja na hayo Masauni alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kutatua kero za wananchi, hivyo Idara ya Uhamiaji iwe mstari wa mbele kuwatumikia wananchi kwa uaminifu na weledi na kuhakikisha kero zote za wananchi zinatafutiwa ufumbuzi.
(Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
 
 

Back to Top