Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

ZOEZI LA UHAKIKI NA UHUISHAJI WA VYETI VYA USAJILI WA TAASISI ZOTE ZA DINI KANDA YA KASKAZINI

 TANGAZO

 Ofisi ya Msajili wa Jumuiya, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itaendesha zoezi Maalum la Uhakiki na Uhuishaji wa Vyeti vya Usajili wa Taasisi za Kidini zilizosajiliwa na Wizara hii, katika Kanda ya Kaskazini inayojumuisha Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha,Tanga, na Manyara kuanzia tarehe 12 mwezi Desemba 2022 saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni.

Viongozi wa taasisi za dini wanahimizwa kufika kwenye Kituo cha Uhakiki na Uhuishaji wa Vyeti vya Usajili kitakachokuwa kwenye Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda  (TRITA) kilichopo Moshi Mjini Mkoani Kilimanjaro wakiwa na:-.

·         Cheti cha Usajili pamoja na nakala ya cheti hicho

·         Katiba na Kanuni zinazotumika.

·         Taarifa za Mapato na Matumizi na Utendaji za  miaka mitano.

·         Uthibitisho wa malipo ya ada kwa miaka mitano, na

·         Ada ya cheti kipya shilingi 100,000.

Taasisi za kidini zitakazoshindwa kushiriki zitahesabika hazipo  hai  hivyo kujiondoa zenyewe kwenye Kanzidata ya Jumuiya zilizosajiliwa .

Huduma za Ulipaji wa Ada zitatolewa, Kanda itakayofuata ni Kanda ya Ziwa na ratiba ya Kanda nyingine itatangazwa baadae.

Kwa ufafanuzi piga namba 0734712744, 0734712745 au barua pepe rs@moha.go.tz.    

Imetolewana:

MSAJILI WA JUMUIYA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI