Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE (NUU) YAKAGUA UJENZI WA KITUO CHA POLISI IKUNGIKamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imekagua na kuridhishwa na utekelezaji wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi kilichojengwa katika Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.

Hayo yameelezwa leo Novemba 12, 2023 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Vita Kawawa (Mb) wakati ilipoambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini (Mb), kukagua Ujenzi wa Kituo hicho.

Kamati imejionea hali ya Ujenzi ikiwa katika hatua za ukamilishaji na kupokea baadhi ya changamoto ambazo ni pamoja na ukosefu wa Samani.

Awali baada ya kuwasili Mkoani humo Kamati hiyo ikiwa imeambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara hiyo Bi. Miriam Mmbaga kwa niaba ya Katibu Mkuu na Watendaji wengine wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ilipokelewa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskasi Muragili, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa