Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

DKT. MADUHU KAZI AIWAKILISHI NCHI MKUTANO WA KIMATAIFA WA BARAZA LA IOM JIJINI GENEVA NCHINI USWISI



NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi (kushoto), akiwa na Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu Geneva, Hoyce Temu @hoyce_temu, katika Mkutano wa 114 wa Baraza la Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), ulioanza Novemba 27, 2023, Geneva nchini Uswisi na Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dkt.Maduhu kazi anaongozwa Ujumbe huo katika Mkutano huo wa siku tatu ulioanza Novemba 27 na utaisha Novemba 29, 2023.

Athari Za Mabadiliko ya Tabia Nchi na vita zinazoendelea duniani, zimeendelea kuongeza Wahamaji Duniani na Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zinazopokea Wahamaji kutoka nchi jirani. Naibu Katibu Mkuu, Dkt Kazi atawasilisha Ujumbe wa nchi leo Novemba 28, 2023 katika Baraza hilo ambapo linaongozwa na Mkurugenzi wake, Bi Amy Pope.