Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

SERIKALI KUONGEZA AJIRA JESHI LA POLISI NCHINISERIKALI KUONGEZA AJIRA JESHI LA POLISI NCHINI.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ALLY GUGU amesema Serikali ina mpango wa kuajiri askari wapya wa Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama nchini


Amesema hayo Juni 28, 2024 katika Kambi ya Kilele Pori iliyopo wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro wakati akifunga mafunzo ya uongozi mdogo ngazi ya Koplo kozi yaliyoendeshwa na Shule ya Polisi Tanzania wilayani Moshi


Katibu Mkuu amewataka Wahitimu wote kuwa na nidhamu na kusimamia askari wa chini yao kutenda kazi kwa weledi


Aidha, amewataka kutambua dhamana iliyopewa Jeshi la Polisi katika kulinda na kusimamia usalama nchini na kuwataka kujiepusha na vitendo vya rushwa 

Naye Naibu Kamishna wa Polisi Anthony Rutashuburugukwa amewataka wahitimu wote kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia misingi yote kama walivyofundishwa na kujiendeleza kwa kupata mafunzo mbalimbali ili kuongeza ujuzi na maarifa yatakayoboresha utendaji ndani ya Jeshi la Polisi nchini.