News

Hotuba ya Mgeni Rasmi

Friday, February 19, 2016

HOTUBA YA MGENI RASMI, WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MHE. CHARLES M. KITWANGA, MB AKIFUNGUA KIKAO CHA KAZI CHA  MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI UKUMBI WA JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVENTION CENTRE, DAR ES SALAAM  TAREHE 18 – 19 FEBRUARI 2016

  • Inspekta Jenerali wa Polisi, Ndugu Ernest Jumbe MANGU,
  • Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdurahman KANIKI,
  • Makamishna wa Polisi,
  • Naibu Makamishna wa Polisi,
  • Wajumbe wa Mkutano,
  • Waandishi wa Habari,
  • Wageni waalikwa,
  • Mabibi na Mabwana.

 
Habari za asubuhi!
Heri ya Mwaka Mpya!
Napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana hapa leo hii. Pili, natumia nafasi hii kumshukuru Inspekta Jenerali wa Polisi ndugu Ernest Mangu kwa kunipa heshima hii ya kuwa Mgeni Rasmi katika Kikao hiki muhimu. Kupitia hafla hii ninapata fursa ya kuzungumza na na viongozi wote waandamizi wa Jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi ambao ni wasimamizi wakuu wa kazi za Polisi. Ninawapongeza sana kwa utaratibu huu mliojiwekea...

Meja Jenerali Rwegasira ataka Polisi wenye tabia ya kuwabambikizia kesi wananchi wachukulie hatua kali

Wednesday, January 27, 2016

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amewataka viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi nchini kuhakikisha wanawachukulia hatua kali askari polisi wenye tabia ya kuwabambikizia kesi wananchi.
Meja Jenerali Rwegasira alisema Jeshi hilo lina sifa nzuri nje ya nchi pamoja na hapa nchini lakini kuna baadhi ya askari wasiowaadilifu wanawaonea wananchi mitaani wasiokuwa na hatia kwa kuwabambikizia kesi ambapo wanalitia doa jeshi hilo.
“Jeshi letu lina sifa nzuri, niliwahi kwenda nchini Kenya nikaambiwa Jeshi la Polisi Tanzania lina maadili kwani hata likimkamata mhalifu linafuata sheria na utaratibu na sio kutumia nguvu kubwa kama yalivyo majeshi mengine,” alisema Rwegazira.
Rwegasira aliongeza kuwa, amefurahishwa sana na utendaji kazi wa jeshi hilo na kutaka kuongeza umakini zaidi ili kuliletea sifa zaidi jsehi hilo na yeye yupo karibu nao katika kuliendeleza jeshi hilo ili liweze kufanya kazi kwa weledi.
Alisema kuwa ni askari wachache mno wenye tabia hiyo ya kuwabambikizia kesi wananchi na kutofuata sheria za jeshi, hivyo kazi ya kupambana na askari hao inawezekana endapo viongozi wa jeshi wakiamua kulifanyia kazi.
“Utendaji kazi wenu ni mzuri, nawapongeza sana hasa mlivyosimamia uchaguzi mkuu vizuri kwani wananchi wengi walikuwa na wasiwasi kuhusu usalama wao katika kipindi cha uchaguzi, lakini mlisimama imara kuhakikisha uchaguzi unamalizika salama,” alisema Rwegasira.
Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa...

Pages

Subscribe to
Back to Top