Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliundwa tarehe 15 Desemba mwaka 1961 baada ya tanganyika kupata uhuru. Kuanzishwa kwa Wizara hii kulilenga kuunda chombo ambacho kingesimamia maswala ya ulinzi na usalama waraia na mali zao katika mazingira ya nchi huru. Chombo hiki kimewezesha nchi yetu kuondokana na sera za kikoloni ambazo ziliznzishwa kwa ajiri ya kulinda maslai ya wakoloni. Majukumu ya Wizara yalitekelezwa kwa kupitia Jeshi la Polisi Idara ya Magereza.
Add new comment