Nini historia ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi?

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliundwa tarehe 15 Desemba mwaka 1961 baada ya tanganyika kupata uhuru. Kuanzishwa kwa Wizara hii kulilenga kuunda chombo ambacho kingesimamia maswala ya ulinzi na usalama waraia na mali zao katika mazingira ya nchi huru. Chombo hiki kimewezesha nchi yetu kuondokana na sera za kikoloni ambazo ziliznzishwa kwa ajiri ya kulinda maslai ya wakoloni. Majukumu ya Wizara yalitekelezwa kwa kupitia Jeshi la Polisi Idara ya Magereza.

Polisi jamii ni nini?

Ni mpango wa kuwashirikisha wananchi katika masuala ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kwa wananchi wenyewe kushiriki katika kujilinda wenyewe.

Ninataka kusajili chama,nifanyaje?

Fuata hatua zifuatazo;
 
1. Fika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mtaa wa Ohio/Ghana
 
2. Utapewa fomu ambayo itakuhitaji uijaze kikamilifu
 
3. Baada ya hapo utarejesha kwa Afisa Sheria wa Wizara ili aweze kukusajili endapo umefuata sheria ya ujazaji wa fomu hiyo.
 
Fomu ya maombi ya usajili bonyeza fomu za maombi

Back to Top