Services

 • Kulinda usalama wa raia na mali zao

  Jukumu kubwa la Jeshi la Polisi ni kuhakikisha usalama na ulinzi wa raia na mali zao kwa kutunza amani na usalama, kutunza sheria na utulivu, kuzuia na kutambua uhalifu, kukamata na kutunza wahalifu na kulinda mali. Idara za Jeshi la Polisi ni pamoja na:

 • Kuhifadhi na kuwarekebisha wafungwa

  Jukumu kubwa la Jeshi la Magereza ni kutunza katika hali salama aina zote za wafungwa na kusimamia urekebishwaji wao. Divisheni za Jeshi la Magereza ni:

 • Kusimamia masuala ya Zimamoto na Uokoaji

  Majukumu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ni kukinga na kupunguza idadi ya vifo, majeraha kwa watu, na uharibifu wa mali kutokana na moto, mafuriko, matetemeko, ajali za barabarani na majanga mengine.
  Idara na Vitengo vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ni pamoja na:

 • Kuwezesha na kusimamia utokaji na uingiaji nchini wa raia na wageni

  Jukumu la Idara ya Uhamiaji ni kuwezesha na kudhibiti utokaji na uingiaji nchini wa raia na wageni kufuatana na Sheria Na. 7 ya 1995, Sheria ya Uraia wa Tanzania Na. 6 ya 1995 na Sheria ya Pasi na Nyaraka za Kusafiria Na. 20 ya mwaka 2002 na Kanuni zinazoambatana na Sheria hizo.
  Divisheni, Vitengo na Ofisi za Idara za Uhamiaji ni pamoja na:

 • Kutoa huduma kwa wakimbizi waliopo nchini

  Jukumu la Idara ya Wakimbizi ni kusimamia masuala ya wakimbizi kufuatana na Sheria ya Wakimbizi ya mwaka 1998 na Sera ya Taifa ya Wakimbizi ya mwaka 2003.
  Sehemu za Idara ya Wakimbizi ni:

  1. Sehemu ya Operesheni na Usalama;
  2. Sehemu ya Sheria na Ulinzi; na
  3. Sehemu ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu.

  Idara hii inangozwa na Mkurugenzi akisaidiwa na Wakurugenzi Wasaidizi.

 • Kusimamia Programu ya Huduma kwa Jamii

  Jukumu la Idara ya Probesheni na Huduma kwa Jamii ni kusimamia adhabu mbadala katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi chini ya Sheria ya Probesheni ya Wahalifu (Kifungu. 247 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002), Sheria ya Huduma kwa Jamii Na. 6/2002, Kanuni ya Kifungo cha Nje ya mwaka 1968 (EML) na Sheria ya Bodi za Paroli Na. 25/1994.
  Sehemu ya Idara hii ni:

  1. Sehemu ya Probesheni
  2. Sehemu ya Huduma za Utunduizi

  Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi akisaidiwa na Wakurugenzi Wasaidizi.

 • Kujenga na kusimamia Mfumo wa Utambuzi na Usajili wa Watu na kutoa Vitambulisho vya Taifa kwa raia na wageni wenye miaka 18 na kuendendea

  Kujenga na kusimamia Mfumo wa Utambuzi na Usajili wa Watu na kutoa Vitambulisho vya Taifa kwa raia na wageni wenye miaka 18 na kuendendea

 • Kushughulikia Malalamiko

  Jukumu ya Idara ya kushughulikia Malalamiko ni kupokea na kushughulikia malalamiko yanayohusu utendaji wa Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Taasisi nyingine zilizo katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Taasisi Binafsi za Ulinzi.
  Sehemu za Idara za Malalamiko ni:

  1. Sehemu ya kushughulikia Malalamiko;
  2. Sehemu ya Sheria na Utafiti.

  Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi.

 • Usajili wa Vyama vya Kijamii

  Jukumu la Idara ya Huduma za Sheria ni kutoa huduma za kisheria kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Sehemu ya Idara ya Huduma za Sheria ni:

  1. Sehemu ya Usajili wa Vyama vya Kijamii;
  2. Sehemu ya Huduma za Kisheria.

  Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi.

Back to Top