Kuhifadhi na kuwarekebisha wafungwa

Jukumu kubwa la Jeshi la Magereza ni kutunza katika hali salama aina zote za wafungwa na kusimamia urekebishwaji wao. Divisheni za Jeshi la Magereza ni:

  1. Divisheni ya Sheria na Shughuli za Magereza;
  2. Divisheni ya Huduma ya Urekebishaji;
  3. Divisheni ya Fedha na Utawala.

Vitengo vya Jeshi la Magereza ni pamoja na Kitengo cha Intelijensia na Operesheni na Kitengo cha Ukaguzi wa Magereza.  Jeshi la Magereza pia lina Shirika la Uzalishaji na Ofisi za Magereza za Mikoa na Wilaya.
Jeshi la Magereza linaongozwa na Kamishna Jenerali wa Magereza akisaidiwa na Makamishna wa Divisheni mbalimbali na Vitengo.
Tembelea Idara ya Magereza www.magereza.go.tz

Back to Top