Kuwezesha na kusimamia utokaji na uingiaji nchini wa raia na wageni

Jukumu la Idara ya Uhamiaji ni kuwezesha na kudhibiti utokaji na uingiaji nchini wa raia na wageni kufuatana na Sheria Na. 7 ya 1995, Sheria ya Uraia wa Tanzania Na. 6 ya 1995 na Sheria ya Pasi na Nyaraka za Kusafiria Na. 20 ya mwaka 2002 na Kanuni zinazoambatana na Sheria hizo.
Divisheni, Vitengo na Ofisi za Idara za Uhamiaji ni pamoja na:

  1. Divisheni  ya Pasi, Uraia na Utaifa;
  2. Divisheni ya Visa, Pasi na Vibali;
  3. Divisheni ya Usimamizi na Uthibiti wa Mipaka;
  4. Ofisi ya Zanzibar;
  5. Divisheni ya Utawala, Fedha na Uhasibu;
  6. Kitengo cha Sheria;
  7. Chuo cha Taaluma za Uhamiaji Tanzania; na
  8. Ofisi za Uhamiaji za Mikoa.

Idara ya Uhamiaji inaongozwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akisaidiwa na Makamishna na Wakuu wa Vitengo.
Tembelea Idara ya Uhamiaji www.immigration.go.tz

Back to Top