Get Adobe Flash player
 • VODACOM YAMKABIDHI WAZIRI CHIKAWE MAMILIONI YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

  Vodacom yamkabidhi Waziri Chikawe Mamilioni kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kupokea hundi ya Sh. Milioni 40 kwa ajili ya maandalizi ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, kutoka kwa Ofisa wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (watatu kulia). Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani  inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, jijini Arusha. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Wapili kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, na kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.

 • Waziri Chikawe Kufuta Usajili wa Makanisa Yenye Migogoro kwa Lengo la Kuepusha Uvunjifu wa Amani Nchini

  Waziri Chikawe Kufuta Usajili wa Makanisa Yenye Migogoro kwa Lengo la Kuepusha Uvunjifu wa Amani Nchini. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na maelfu ya Waumini wa Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa yaliyofanyika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam. Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo aliyataka Makanisa nchini kudumisha amani na utulivu na kuendelea kuliombea Taifa na kuepuka kuingia katika migogoro mbalimbali ambayo itasababisha taifa kuingia katika uvunjifu amani makanisani.

 • Maonesho ya Kimataifa ya Biashara sabasaba

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (aliyevaa tai) akiongozwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soko la Ndani, Edwin Rutageruka (watatu kulia) kuelekea kuangalia usalama katika sehemu mbalimbali ya Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba). Nyuma ya Waziri Chikawe upande wa kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (wapili kulia). Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea viwanja hivyo vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, kuangalia hali ya usalama katika viwanja hivyo.

 • Maonesho ya Kimataifa ya Biashara sabasaba

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akikiangalia cheti cha usajili wa vyama katika Banda la Wizara yake wakati wa Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea viwanja hivyo vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, kuangalia hali ya usalama katika viwanja hivyo. Kushoto ni Afisa Sheria, Flora Mlope ambaye alikuwa akitoa maelezo ya usajili wa vyama

 • Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

  Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Mathew Ikomba akitoa maelezo ya namna Idara hiyo ilivyofanikiwa kutumia teknolojia  mpya  ya utoaji wa vibali vya ukaazi kwa mfumo wa kielectroniki na hivyo kuondokana na mfumo wa awali wa kuandika vibali hivyo kwa mkono,  mbele ya   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe  wakati Waziri huyo alipotembelea Mabanda ya Wizara yake katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

 • Image5

  Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Loyce Abeid, akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto) kifaa kinachotumika kwa ajili ya uokozi wa magari yanapopata ajali hasa magari ya tenki. Malemi alitetembelea Banda la Wizara na Taasisi zake katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

 • Image2

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza kwa makini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (katikati) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu ya Zanzibar

 • Image3

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akitoa hotuba fupi ya kuishukuru Serikali ya Japan kwa kuisadia wizara yake kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji magari matano kwa ajili ya kazi ya kuzima moto na uokoaji nchini.

 • Image7

  Msimamizi wa Kiwanda cha Kuzalisha Nyuzi za Mkonge cha Gereza Kihonda lililopo mkoani Morogoro, Fidelis Muhaya akimuonyesha majani ya mkonge ambayo yamevunwa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (Kushoto). Katikati ni Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Sekta ya Sheria nchini, Wanyenda Kutta.

 • Image4

  Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, akiangalia moja ya hati zinazotolewa na Uhamiaji, wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Pereira Ame Silima.