Serikali ya Tanzania imeweka wazi Mpango wake wa kutotoa Uraia kwa Wakimbizi wanaoishi katika kambi za Wakimbizi zilizopo hapa nchini huku ikiwataka wakimbizi hao kuwa tayari kurejea nchini Burundi ambako imehakikishiwa kurejea kwa Hali ya Amani na Utulivu.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2025 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene wakati wa Mkutano wa 26 wa Pande Tatu baina ya Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) uliohusu Urejeshaji Wakimbizi katika nchi yao ya Burundi.