Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

RAIS SAMIA AIPONGEZA WIZARA YA MAMBO YA NDANI, KINARA MICHEZO YA MEI MOSI 2025.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. DKt.  Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ushindi wa ujumla katika Mashindano ya michezo ya Mei Mosi 2025.


Rais Samia alitoa pongezi hizo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yaliyofanyika kitaifa katika Uwanja wa Bombadia mkoani Singida, leo tarehe 01 Mei 2025.


“Niwapongeze wanamichezo wote na kwa umaalumu kabisa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, leo wamekusanya zawadi nyingi sana, kwa hiyo nawapongeza kwa dhati,” alisema Rais Samia.


Aidha, Rais Samia aliwahimiza wafanyakazi wote kuzingatia masuala ya michezo mahala pa kazi, akisisitiza kuwa michezo ni afya.