Tanzania logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

WANAFUNZI 300, WAPATIWA ELIMU YA KUPAMBANA NA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU


Maafisa wa Sekretarieti  ya  Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu,iliyopo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wametoa elimu  kuhusu Mapambano ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu kwa wanafunzi na walimu wa shule ya Sekondari Zuzu iliyopo wilaya ya Dodoma Mjini, katika Jiji la Dodoma. 


Elimu imetolewa kwa wanafunzi 300 na walimu 6 wa shule hiyo na kuaswa kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya uhalifu huo kwa kutoa taarifa kupitia No ya dharura 195.


Elimu hiyo imekuwa ya manufaa makubwa na kuwafanya wanafunzi na walimu kuomba nafasi ya kupatiwa elimu hii kwa wakati mwingine.