Tanzania logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Maelezo Kuhusu Wizara

Kwa mujibu wa Hati ya Mgawanyo wa Majukumu ya Wizara kama ilivyotolewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akikidhinisha Muundo Mpya na Mgawanyo wa Majukumu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mnamo Januari 2021, katika hati hii, Mhe. Rais ameunda Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi yenye jukumu la kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Sera za Usalama wa raia, Uhamiaji, Wakimbizi, Huduma za Zimamoto na Uokoaji, Huduma za Magereza, Huduma za Uhamiaji na Uraia, Usajili na Urati bu wa Jumuiya na Taasisi zisizo za Kiserikali (NGO’s), Uraia, Utambuzi wa Watu, Huduma za Wakimbizi, Huduma za Zimamoto na Uokoaji, Uangalizi, Parole na Huduma za Kijamii, Urejeaji, uboreshaji wa utendaji wa maendeleo ya rasilimaliwatu, Idara saidizi, Mamlaka, Miradi na program chini ya Wizara.