Idara na Vitengo
KUHUSU IDARA YA HUDUMA KWAWAKIMBIZI
Idara ya Huduma kwa Wakimbizi chini ya Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi ilianzishwa mwaka 1997 kwa lengo la kusimamia na kuratibu masuala yote yanayohusu Wakimbizi nchini.
Shughuli za Idara ya Huduma kwa Wakimbizi zinasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya
Wakimbizi ya mwaka 1998, Sera ya Taifa ya Wakimbizi ya mwaka 2003, pamoja na
Mikataba ya Kimataifa (1951 Geneva Convention relating to refugee status and its 1967
Protocol na 1969 OAU Convention Governing the Specific Aspects of Refugee
Problems in Africa). Idara ya Huduma kwa Wakimbizi
inaongozwa na Mkurugenzi.
Chini ya Mkurugenzi, Idara ina vitengo vinne
ambavyo vinaongozwa na Wakurugenzi Wasaidizi, Vitengo hivyo ni: -
i.
Usalama na Operesheni ;
ii.
Sheria na Hifadhi;
iii.
Usimamizi wa Kambi na Makazi na
iv. Fedha na Usimamizi wa Miradi.
Aidha, Idara ina ofisi ya Kanda iliyopo mkoani Kigoma inayoongozwa na Mratibu wa Kanda pamoja na Ofisi za Wakuu wa Kambi na Makazi ya Wakimbizi katika Mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi.
MAJUKUMU YA IDARA YA HUDUMA KWA WAKIMBIZI
i.
Kuwapokea, kuwasajili, kuwahifadhi na kuratibu usimamizi
wa huduma zinazotolewa kwa
waomba hifadhi na wakimbizi wanaohifadhiwa hapa nchini;
ii.
Kuwatafutia suluhisho la kudumu
wakimbizi waishio nchini ikiwa pamoja na kuwarejesha nchini kwao au
kuwahamishia nchi ya tatu.
iii.
Kuratibu udhibiti, usalama na
usimamizi wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuhifadhi wakimbizi pamoja na
maeneo ya nje.
iv.
Kusimamia utekelezaji wa Sera,
Sheria na Mikataba mbalimbali ya Kimataifa kuhusu hifadhi ya ukimbizi nchini.
v.
Kusimamia mashirika ya misaada ya
kibinadamu katika hifadhi ya ukimbizi ili kuhakikisha kuwa yanatekeleza
majukumu kwa mujibu wa mikataba iliyosainiwa.
1.
UTANGULIZI
Idara ya Sera na Mipango ni miongoni mwa
Idara nne (4) zilizopo Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Fungu
51). Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango. Aidha, Idara
inaundwa na Sehemu mbili (2) ambazo ni:
(i) Sehemu ya Sera, Utafiti na Ubunifu; na
(ii) Sehemu ya Mipango na Bajeti.
2. MAJUKUMU YA IDARA
Majukumu ya Idara ya Sera na Mipango ni kama ifuatavyo:
(i) Kuratibu maandalizi ya mipango, bajeti na sera za Wizara kwa kuzingatia mfumo wa mipango ya kitaifa;
(ii) Kuchambua sera kutoka sekta nyingine na kushauri ipasavyo;
(iii) Kuratibu utafiti wa sera za Wizara na kazi zinazohusiana na sekta kwa ajili ya maendeleo ya sekta husika;
(iv) Kuratibu utekelezaji wa sera, utafiti, maendeleo ya kiteknolojia na ubunifu katika Wizara;
(v) Kuratibu maandalizi ya hotuba ya bajeti kwa Wizara;
(vi) Kuandaa mwongozo wa masuala ya utafiti na ubunifu kwa Wizara;
(vii) Kufanya utafiti wa utoaji wa huduma za Wizara (Service Delivery Survey);
(viii) Kuratibu tathmini ya Wizara (Institutional Self-Assessment);
(ix) Kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa mipango ya Wizara;
(x) Kuratibu usimamizi wa vihatarishi ndani ya Wizara;
(xi) Kuratibu utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala, Maagizo ya Serikali na masuala ya Bunge; na
(xii) Kuratibu maandalizi ya taarifa za utendaji za Wizara.
2.1. Sehemu ya Sera, Utafiti na Ubunifu
Sehemu hii inaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Sera, Utafiti na Ubunifu. Majukumu yanayotekelezwa na sehemu hii ni yafuatayo:
(i) Kuratibu utungaji na utekelezaji wa Sera za Wizara;
(ii) Kuratibu mapitio ya Sera za Wizara;
(iii) Kuandaa taarifa za utekelezaji wa Sera za Wizara;
(iv) Kupitia na kushauri kuhusu nyaraka za sera zilizoandaliwa na Wizara nyingine;
(v) Kuandaa mwongozo wa masuala ya utafiti na ubunifu ya Wizara;
(vi) Kuratibu masuala ya utafiti na ubunifu ili kufanya maamuzi sahihi;
(vii) Kuratibu usimamizi wa masuala ya ubunifu kwa Wizara;
(viii) Kushirikiana na taasisi za utafiti na vituo vya takwimu za kitaifa na kimataifa kwa lengo la kukusanya na kubadilishana taarifa za utafiti na ubunifu;
(ix) Kubainisha maeneo ya utafiti na vipaumbele kwa Wizara; na
(x) Kuandaa mikakati ya utekelezaji na usambazaji wa matokeo ya utafiti.
2.2. Sehemu ya Mipango na Bajeti
Sehemu hii inaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Bajeti. Majukumu yanayotekelezwa na Sehemu ya Mipango na Bajeti ni kama ifuatavyo:
(i) Kuratibu maandalizi ya Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Wizara, mipango kazi na bajeti;
(ii) Kuratibu maandalizi ya Hotuba ya Bajeti ya Wizara;
(iii) Kufanya mapitio ya mipango na programu zinazotekelezwa katika Wizara;
(iv) Kuratibu maandalizi ya taarifa za utendaji kwa ajili ya Wizara;
(v) Kuratibu utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala, maelekezo ya Serikali na masuala ya Bunge;
(vi) Kuandaa mikakati ya utafutaji wa rasilimali kwa ajili ya Wizara;
(vii) Kuandaa nyaraka za miradi na programu kwa ajili ya ugharamiaji;
(viii) Kutoa mwongozo na msaada wa kitaalam kwa ajili ya kuanzisha mipango mkakati na taratibu za bajeti ndani ya Wizara;
(ix) Kufanya utafiti kwa ajili ya utoaji wa huduma za Wizara;
(x) Kuratibu tathmini ya Wizara (tathmini ya kitaasisi);
(xi) Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa usimamizi wa vihatarishi kwa ajili ya Wizara;
(xii) Kuratibu uandaaji wa programu na miradi ya Wizara.
A UTANGULIZI
Sekretarieti imeanzishwa chini ya
Kifungu cha 30 (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa
Binadamu Sura ya 432. Sekretarieti iko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi na ina jukumu la Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu
ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuratibu na kushirikiana
na Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali katika masuala ya
kuzuia, kuwaokoa na kuwalinda wahanga, kufanya uchunguzi na kuendesha mashtaka.
Taarifa nyingine kuhusu Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu
· Kuanzishwa
kwa kituo cha Huduma kwa wateja kupitia simu (CALL CENTRE) ambapo wananchi wote
wataweza kupiga namba maalum ya dharura 195
kwa ajili ya kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu wa Usafirishaji Haramu wa
Binadamu. Namba hii ni bure haina gharama yoyote pindi mwananchi atakapokuwa
akipiga namba hiyo;
· Kuanzisha
Kanzidata ya Kitaifa ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu (TIPMIS) ambayo
itaunganishwa kwenye mfumo jumuishi wa masuala ya Haki Jinai Tanzania.