WAZIRI KATAMBI AKUTANA NA BALOZI WA CHINA MHE. CHEN
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Patrobas Katambi amekutana na Balozi wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Chen Mingjian na kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo ushirikiano Kati ya Nchi hizo mbili katika masuala mbalimbali ya Kudhibiti uhalifu na matumizi ya teknolojia katika masuala ya Usalama ikiwemo udhibiti wa uhalifu unaovuka mipaka.
Mazungumzo hayo pia yamehudhuriwa na Mkuu wa Huduma za Urekebu kutoka Jeshi la Magereza,Kamishna Amina Kavirondo na Afisa Kiungo wa China, Kitengo cha Polisi Kimataifa,Makao Makuu ya Upelelezi,Mrakibu wa Polisi,SP Damas Nyungula.
Majadiliano hayo yamefanyika Ofisi ndogo ya waziri,jijini Dar es Salaam
