Tanzania logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

UHAMIAJI YADHIBITI VIPENYO 1,777


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi amesema katika kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia nchini. Idara ya Uhamiaji imedhibiti na kufunga jumla ya Vipenyo Elfu Moja Mia Saba Sabini na Saba vilivyopo maeneo mbalimbali nchini, vilivyokua vinatumika kuingia nchini  kwa njia hiyo isiyo halali.


Ametoa kauli hiyo wakati wa ziara iliyofanyika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, jijini Dodoma ambapo pia aliongozana na Naibu Waziri Ayoub Mohamed Mahmoud ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo Naibu Waziri na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala pia walipata nafasi ya kutoa neno.


“Mmeendelea Kudhibiti vipenyo ambavyo vipo zaidi ya 1.777 unaweza ukaona kazi kubwa ambayo mmeifanya Kwenye maeneo rasmi ya mipaka yetu,kwenye boda mpo lakini pia kwenye maeneo ya boda za maji mpo,lakini pia nchi kavu na angani na Kwenye viwanja vya ndege,niwapongeze kwa udhibiti wenu imara pamoja na changamoto mbalimbali ambazo zipo,ndio maana tunataka tuongeze magari na vitendea kazi ili muweze kufanya vizuri zaidi.Niwaahidi tutaanza kuangalia kwenye maeneo yenye teknolojia ya kisasa tutaiga na tutaenda kujifunza.” alisema Katambi 


Akizungumza katika ziara hiyo,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Ayoub Mohamed Mahmoud alisema idara ya uhamiaji sio tu mlinzi wa mipaka bali ni Kituo cha kimkakati kinachoathiri usalama wa taifa heshima ya kimataifa endapo hakitafanya kazi ipasavyo huku akianza na pongezi akiwapongeza idara hiyo kwa kazi nzuri sambamba na kuijengea Nchi heshima.


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewapa kibali cha kuajiri na upandishaji vyeo huku jumla ya askari 557 kwa mwaka 2025 na sasa hivi ndani ya mwaka huu wako kwenye mchakato wa ajira watu 454 ambapo alimshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwaongezea nguvu kazi ya askari wa uhamiaji.