Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema itahakikisha uhamiaji salama ili kulinda usalama wa nchi, raia, mali,usalama wa kikanda na usalama wa kimataifa huku ikisisitiza maendeleo ya Uchumi, Ajira, Utamaduni, Siasa yatafanyika bila kuathiri usalama na kulinda tunu ya amani na kuzingatia haki za binadamu.Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi wakati akizindua Mfumo wa Uratibu wa Kitaifa kuhusu Uhamiaji Nchini