TANZANIA YASISITIZA UHAMIAJI SALAMA ILI KULINDA AMANI
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema itahakikisha uhamiaji salama ili kulinda usalama wa nchi, raia, mali,usalama wa kikanda na usalama wa kimataifa huku ikisisitiza maendeleo ya Uchumi, Ajira, Utamaduni, Siasa yatafanyika bila kuathiri usalama na kulinda tunu ya amani na kuzingatia haki za binadamu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi wakati akizindua Mfumo wa Uratibu wa Kitaifa kuhusu Uhamiaji Nchini Tanzania huku Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji(IOM), Amy Pope akiishukuru Serikali ya Tanzania kwa kutafuta suluhisho sahihi juu ya uhamiaji ili kuwepo na uhamaji unaofuata sheria na taratibu.
“uhamiaji ni masuala ya usalama wa raia na mali zao,usalama wa nchi,usalama wa kikanda na Kimataifa na ndio maana Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ina dhamana katika hili lakini majukumu ya kiuchumi yanalazimu mtu aweze kwenda maeneo mbalimbali kutafuta ajira, fursa lakini haya yote yafanyike bila kuathiri usalama wa nchi husika, uchumi wa nchi husika bila kuathiri raia wa nchi husika” amesema Waziri Katambi
