WAZIRI KATAMBI MBELE YA KAMATI YA NUU KUWASILISHA UTEKELEZAJI WA UHAMIAJI NA NIDA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amewasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) na Masuala ya Idara ya Uhamiaji.
Waziri Katambi amewasilisha taarifa hizo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama,Bungeni jijini Dodoma.
Akiongea baada ya mawasilisho hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama,Najma Murtaza Giga ameipongeza wizara kwa kuendelea kusimamia maono ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha amani na utulivu unaendelea kuwepo nchini.
Kamati mbalimbali za Bunge ziko katika vikao na Watendaji wa Serikali na Idara ili kupokea Taarifa za Utekelezaji kuelekea Kikao cha Bunge kinachotarajiwa kuanza hivi Karibuni.
