WAZIRI SIMBACHAWENE AONGOZA KIKAO KAZI NA VIONGOZI WA JESHI LA POLISI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene, ameongoza kikao kazi na viongozi wa Jeshi la Polisi nchini kilichofanyika jijini Arusha leo Novemba 21, 2025 ikiwa ni mara yake ya kwanza kuongoza kikao hicho baada ya uteuzi wake wa kuongoza Wizara hiyo
Katika kikao hicho, Waziri Simbachawene ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Denis Londo, pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Maduhu Kazi.
