MAGEREZA BORESHENI UFANISI:KATIBU MKUU
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Senga Gugu ameliagiza Jeshi la Magereza nchini Kuongeza ufanisi katika shughuli zake za uzalishaji ikiwemo kilimo,ufugaji na uzalishaji wa bidhaa za viwandani huku akilitaka jeshi hilo kuhakikisha linazalisha mazao kwa wingi na kuuza ndani na nje ya mipaka ya Tanzania baada ya kukamilisha jukumu la kulisha askari magereza na wafungwa.
Ametoa rai hiyo wakati wa Ziara ya Ukaguzi wa Mazao ya Mahindi yaliyovunwa katika Gereza la Kilimo la Songwe na Gereza la uzalishaji wa sabuni katika Gereza la Ruanda mkoani Mbeya.
