Tanzania logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

KATIBU MKUU GUGU AFUNGUA MAFUNZO YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA VIHATARISHI


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ally Gugu amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo kuhakikisha wanakuwa na uelewa wa pamoja katika kutambua, kutathmini na kudhibiti Vihatarishi vinavyoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa majukumu yao


Gugu amezungumza hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Siku mbili ya masuala ya usimamizi na udhibiti wa Vihatarishi kwa Wakuu wa Idara na Vitengo yaliyofunguliwa rasmi leo mkoani Morogoro Oktoba 9, 2025


"Kwa kuzingatia kuwa suala la Vihatarishi bado ni geni katika Taasisi nyingi za Umma Uongozi wa Wizara umeona ni vema Menejimenti yake ikapata Mafunzo kuhusu suala hili" Amesema Gugu 


Aliongeza kuwa Mafunzo hayo ya siku mbili kwa Menejimenti ya Wizara yatawaongezea uelewa kuhusu Vihatarishi vilivyopo katika Maeneo yao ya kazi na namna ya kuweza kuvidhibiti ili kuhakikisha malengo ya Wizara hiyo yanafikiwa kama yalivyokusudiwa


Aidha amepongeza Kitengo cha Divisheni ya Sera na Mipango kwa uratibu wa Mafunzo hayo Muhimu kwa Menejimenti ya Wizara sambamba na kuishukuru Wizara ya Fedha ambayo wakati wote imekua pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kuhakikisha Wizara inapata Mafunzo ya Usimamizi na udhibiti wa Vihatarishi