TIMU YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YASHIRIKI MICHEZO YA KIRAFIKI BAGAMOYO

Timu ya Michezo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeshiriki michezo ya kirafiki na timu ya Wilaya ya Bagamoyo, Michezo hiyo imehusisha Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete, Agosti 9, 2025 ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mshikamano na kujenga mahusiano ya kijamii kupitia michezo
Baada ya michezo hiyo Washiriki hao wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bi. Miriam Mbaga pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara walitembelea Gereza la Kigongoni na kukabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali kwa uongozi wa Gereza hilo.
Aidha walifika katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Moyo Mmoja kilichopo wilayani Bagamoyo na kutoa msaada wa vyakula na mahitaji mengine muhimu kwa watoto wanaolelewa kituoni hapo, kama sehemu ya mchango wa kijamii kupitia michezo.
Katika hatua nyingine, Washiriki hao walitembelea Makumbusho ya Caravan Sites pamoja na fukwe za bahari za Bagamoyo, ambapo walipata nafasi ya kujifunza mambo mbalimbali ya kihistoria katika mkoa huo wa Pwani