Tanzania logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. AYOUB ASHIRIKI MKUTANO WA KAMATI YA MAWAZIRI WA ASASI YA SIASA, ULINZI NA USALAMA NCHINI MALAWI


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, ameshiriki Mkutano wa 28 wa wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika leo, nchini Malawi.


Mhe. Ayoub ameshiriki mkutano huo akiwa sehemu ya ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. James Millya


Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri na Makatibu Wakuu, pamoja na Wawakilishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka nchi wanachama wa SADC kujadili masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika kudumisha amani, utulivu na usalama, pamoja na kutafuta suluhisho la changamoto zinazoikabili kanda ya Kusini mwa Afrika.


Akifungua mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi George Chakonda, amesisitiza umuhimu wa nchi wanachama kuendelea kushirikiana katika kuimarisha amani, usalama na utawala bora, ikieleza kuwa mafanikio ya SADC yanategemea mshikamano, ushirikiano na dhamira ya pamoja ya kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wa ukanda huo.