Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

WIZARA NNE ZATEMBELEA SHULE YA POLISI MOSHI



Makatibu Wakuu wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Maji pamoja na Wawakilishi wa Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha na Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  leo wamefanya  ziara ya pamoja kutembelea Shule ya Polisi Tanzania- Moshi na kukagua miundombinu iliyopo katika  Kambi ya Kilele  Pori na  Kamba Pori Kilimanjaro ili kubaini Changamoto na  kuweka Mikakati ya pamoja ya kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili Kambi hizo.

Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Kaspar  Mmuya  aliyeambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof.Jamal  Katundu, Wawakilishi wa Makatibu Wakuu  Wizara ya Fedha na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Awadhi Juma Haji na baadhi ya Watendaji wa Jeshi la Polisi kwa pamoja wamekagua miundombinu mbalimbali iliyoko katika Kambi ya Kilele Pori na Kamba Pori na kuweka mikakati ya pamoja ya  kutatua changamoto zilizobainishwa katika Kambi zote mbili.

Katika Kikao cha pamoja kilichofanyika kwenye Kambi hizo baada ya ukaguzi wa miundombinu,   kwa pamoja  Viongozi hao wamekubaliana  kuzitafutia ufumbuzi changamoto zote zilizobainishwa.

Kwa Upande wake Kamishna wa Operesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Awadhi Juma Haji ameipongeza Serikali kwa namna inavyosaidia kutatua changamoto mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi.