Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

KATIBU MKUU MMUYA AKABIDHIWA TUZO



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe: Kaspar Mmuya leo Novemba 02, 2023 amepewa tuzo maalumu ya kutambua utendaji kazi wake mzuri wakati alipokua Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu.

Akikabidhi tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bi. Stella Mwaisaga amesema Mheshimiwa Mmuya alianzisha utamaduni wa kuwapongeza watendaji wa Wizara hiyo pindi wanapofanya vizuri lakini pia kuwafariji pale wanapopata changamoto mbalimbali ikiwemo misiba na magonjwa hali ambayo imeongeza mshikamano miongoni mwao.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Mheshimiwa Kaspar Mmuya mbali na kushukuru kwa kupewa tuzo hiyo, amebainisha kuwa utaratibu wa kuwajali wafanyakazi ni utaratibu mzuri na wenye tija kwa kuwa unawafanya wafanyakazi kuona mchango wao katika taasisi husika.

Makabidhiano hayo ya Tuzo yalishuhudiwa na Mhasibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu.