Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

NAIBU WAZIRI SAGINI APOKEA MAGARI 43 YA POLISI KUTOKA KAMPUNI YA ASHOK LEYLAND.Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini Novemba 21, 2023 amepokea magari 43 kati ya magari 200 yaliyosalia katika mkataba wa magari 800 ulioingia na serikali ya India kupitia fedha kutoka Exim Bank kwa watengenezaji wa magari ya Ashok Leyland wa mwaka 2013.

Akizungumza mara baada ya kupokea magari na kuyanidhi kwa Jeshi la Polisi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini, anasema lengo ni kuliwezesha Jeshi la Polisi kutekeleza majukumu yao ipasavyo kupitia vitendea kazi muhimu ambavyo ni magari.

Aidha Sagini anasema kupitia magari hayo Jeshi la Polisi litaweza kuwafikia wahalifu kwa haraka na Wananchi watapata huduma kwa wakati sahihi.

Akizungumza na Jeshi la Polisi amewaagiza kutenga bajeti kwa ajili ya ukarabati wa magari hayo ili yaweze kutumika miaka mingi na upande wa kampuni ya Ashok amewataka kuweka karakana ambazo zitarahisisha ukarabati wa magari hayo ukijitajika.

Sagini alisema pia magari 157 yaliyosalia hayatachukua muda mrefu yatakuwa yanekabidhiwa kwa maana wapo katika hatua za mwisho za mkataba huo.