Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MAFUNZO MAALUM KWA WAANDISHI WA HABARI MAMBO YA NDANI YA NCHI YAFUNGWA RASMI.Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefunga mafunzo maalum kwa Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali yaliyohusu namna ya kuripoti taarifa za matukio ya Wizara hiyo na Vyombo Vyake vya Usalama, yakiwemo matukio ya Uhalifu na Majanga yanayohitaji Maokozi.

Akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo Desemba 23, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa NSSF, Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bi. Christina Mwangosi
aliwashukuru Waandishi wa Habari kwa kukubali kushiriki katika Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyojumuisha waandishi wa habari wa Social Media, Magazeti, TV

"Natumaini tumejifunza namna ya kuripoti taarifa zinazohusu Wizara yetu na Vyombo vyake vya Usalama kwa kuzingatia taaluma ya uandishi wa habari hii itasaidia sana taarifa tunazoandika na kuchapisha kwenye Vyombo vyetu vya habari kuzingatia miiko ya uandishi wa habari, na weledi alisema Bi. Christina.

Awali Mafunzo hayo ya Siku mbili kwa Waandishi wa Habari yaliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi yalifunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Kaspar Kaspar Mmuya, Desemba 20, 2023 ambapo yamehitimishwa rasmi hii leo