Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

ULIPAJI WA ADA KWA JUMUIYA ZA KIRAIA ZILIZOSAJILIWA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHIOfisi ya Msajili wa Jumuiya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inazikumbusha  Jumuiya za Kidini na zisizokuwa za Kidini zilizosajiliwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kulipa Ada ya Mwaka pamoja na malimbikizo ya ada za miaka ya nyuma kabla ya tarehe 30/6/2023.

 

Jumuiya za Kidini zinapaswa kulipa Ada ya Shilingi 100,000 na Jumuiya zisizo za Kidini zinapaswa kulipa Ada ya Shilingi 50,000. Aidha, ulipaji wa ada unapaswa kwenda sambamba na uwasilishaji wa Taarifa za Fedha zilizokaguliwa na Taarifa za Utendaji  za Jumuiya hizo kwa kipindi cha mwaka 2022/2023.

 

 

Viongozi wa Jumuiya zote zilizosajiliwa wanakumbushwa na kusisitizwa kutumia Mfumo wa Usajili na Usimamizi wa Jumuiya (RSMIS) unaopatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambayo ni www.moha.go.tz kwa ajili ya kulipa Ada za Jumuiya zao au kufika katika Ofisi zetu zilizopo Jengo la Kambarage Ghorofa ya 11 Jijini Dodoma au Jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ghorofa ya Kwanza Jijini Dar es salaam kwa lengo la kupatiwa huduma stahiki.

 

Kwa maelekezo zaidi, piga simu namba 0734 712 744 au 0734 712 745.

 

Imetolewa na:

 

Emmanuel R. M. Kihampa

 

MSAJILI WA JUMUIYA ZA KIRAIA