Tanzania logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

DKT. SAMIA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA 2026 WA MAOFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua Mkutano Mkuu wa Mwaka 2026 wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi.

 Ufunguzi huo umefanyika katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) Moshi, Kilimanjaro, ukihudhiwa pia na vingongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 Pamoja na masuala mengine aliyozungumza katika hafla hiyo, Dkt. Samia, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kutekeleza Programu ya Polisi Jamii ikiwa ni imekuwa ikiendeleza juhudi za kuimarisha ushirikiano na wananchi kupitia hiyo, akilitaka jeshi hilo kuendelea kutumia ushirikiano huo katika kuimarisha usalama na ulinzi wa raia nchini.

Amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha mahusiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi, akieleza kuwa usalama wa nchi ni jukumu linalohitaji ushirikiano wa pamoja kati ya vyombo vya dola na jamii inayovizunguka.

Aidha, pongezi hizo zinaweka msisitizo katika kuendeleza Polisi Jamii kama nyenzo ya kuimarisha ushirikiano wa polisi na wananchi, ili kuongeza uelewa wa masuala ya usalama na kuimarisha mazingira ya amani na utulivu nchini.