KATIBU MKUU GUGU ASISITIZA MATUMIZI YA MIFUMO
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wameaswa kujifunza na kutumia mifumo mbalimbali ikiwemo mfumo wa ujazaji wa majukumu yao ya utendaji katika Mfumo unaotumika Kupima na Kusimamia Utendaji Kazi wa Watumishi wa Umma(PEPMIS) ambapo pia amewaasa kufanya kazi kwa uaminifu,uweledi,ubunifu ili kutimiza jukumu la kulinda raia na mali zao.
Rai hiyo imetolewa leo jijini Arusha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu wakati akifungua Kikao cha Baraza Dogo la Wafanyakazi fungu 51.
Katibu Mkuu pia amewaasa watumishi hao kuwa na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii huku pia akiwasisitiza utunzaji wa taarifa za serikali na taarifa binafsi sambamba na kufuata kanuni na maadili ya utumishi wa umma na kuwa na tabia na mwenendo bora.
Katika Baraza hilo Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi(fungu 51) ya mwaka wa Fedha 2026/2027 kwa kipindi cha kuanzia tarehe 01 Julai,2026 hadi tarehe 30 Oktoba,2026.
