DIVISHENI YA HUDUMA ZA UANGALIZI YATOA ELIMU KWA JESHI LA POLISI WILAYA YA NKASI
Afisa Huduma za Uangalizi wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa Bw. Salum Maganga amepata fursa ya kutoa elimu juu ya adhabu mbadala zinazosimamiwa na Divisheni ya Huduma za Uangalizi iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katika utoaji wa elimu Afisa Huduma za Uangalizi alitoa elimu kuhusu Sheria zinazosimamia majukumu ya Divisheni ambazo ni Sheria ya Huduma za Jamii sura ya 291 na Sheria ya Kifungo cha nje kwa wahalifu sura ya 247.
Aliweza kusisitiza umuhimu wa Jeshi la Polisi katika utekelezaji wa Sheria hizi hasa wao ni wadau muhimu katika utoaji wa taarifa kipindi Cha uchunguzi wa kijamii kwani wao ndio wanahusika katika kufanya upelelezi wa makosa ya Jinai hivyo wanaelewa mhalifu ni mkosaji wa kwanza au wa kujirudia, pia wanajukumu la kuhifadhi wahalifu/watiwa hatiani (reception center) wakati Afisa akifanya uchunguzi, wanajukumu la kukamata wafungwa waliokiuka masharti ya vifungo vya nje na kuwapeleka Mahakamani na Polisi Kata Wana jukumu kubwa la kufanya ufuatiliaji wa tabia wa wafungwa walio katika kata zao.
Jeshi la Polisi lilishukuru kwa elimu hii na kueleza kuwa wako tayari kutoa ushirikiano kwa Divisheni ya Huduma za Uangalizi katika kutekeleza majukumu yake katika wilaya ya Nkasi.
