RWEZIMULA AFANYA ZIARA JESHI LA MAGEREZA
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Franklin Jasson Rwezimula, amefanya ziara ya kwanza ya kujitambulisha katika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dodoma leo na kufanya kikao kazi na viongozi wa jeshi hilo.
Katika ziara hiyo, Dkt. Rwezimula amepata fursa ya kufahamiana na viongozi na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya jeshi hilo.
Naibu Katibu Mkuu amesema Wizara itaendelea kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kuboresha utendaji na kuhakikisha majukumu ya jeshi hilo yanatekelezwa kwa ufanisi.
