ZIARA YA KITUO CHA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA BUJORA
Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,imetembelea Makumbusho ya Taifa ya Bujora yaliyopo jijini Mwanza ambapo walipata kushuhudia mila,desturi na tamaduni za kabila la wasukuma.
Ziara hiyo ni mjumuisho wa Kikao Kazi kilichoanza tarehe
3/11/2026 ambapo Wajumbe wa Menejimenti ya wizara hiyo walikutana jijini Mwanza
katika Kujadili na Kuboresha Utekelezaji wa Majukumu ya kuwahudumia wananchi.
